Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja
MBUNGE wa
Sengerema mkoani Mwanza, William Ngeleja ametangaza rasmi nia yake ya
kuwania urais wa Tanzania, huku akiweka wazi kuwa yeye hakuhusika na
kashfa ya Escrow kwa madai kuwa wapo watu wanaoitumia kashfa hiyo kwa
lengo la kumchafua kisiasa, anaripoti Mwandishi Wetu, Nashon Kennedy,
Mwanza.
Ngeleja
alitangaza nia yake hiyo ya kuwania urais jana jijini hapa katika Ukumbi
wa Chuo cha Benki Kuu (BoT) , akiwa ameongozana na baba yake mzazi
Mganga Ngeleja, mkewe Blandina na mtoto wa Shemeji yake Maria Ntanga.
Sakata la Escrow na maadili
Alisema
kuwa wakati wa Sakata la Escrow yeye alichafuliwa na baadhi ya watu
ingawa hakuweka bayana ni akina nani na kuongeza kuwa suala hilo
lilitolewa ufafanuzi na Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akizungumza na
wazee wa Dar es Salaam mapema mwaka jana.
“ Mimi
katika suala la Escrow, Rais Kikwete alisema ni Sh bilioni 202 tu
zilizobainika katika sakata la Escrow na kwamba zile hazikuwa fedha za
umma bali ni za kampuni binafsi, katika hili kuna watu kwa makusudi
wanaibua hasira za watu na kuwachafua wengine, wapo wanaotumia siasa
kuchafua watu,” alifafanua.
Kuhusu
kuvuliwa wadhifa wa uwaziri kwa ajili ya kubainika katika taarifa ya
Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2012, alisema
kuwa yeye hakuwa na kashfa kupitia ripoti hiyo na kamwe hakuondolewa
uwaziri kwa sababu ya kashfa bali aliondolewa katika mabadiliko ya
kawaida aliyoyafanya Rais Kikwete.
“Wapo
watu wanaodhani katika mabadiliko ya mawaziri aliyoyafanya Rais Kikwete
Desemba 4 mwaka 2012, sikuwa na kashfa yoyote ile, yalikuwa ni
mabadiliko ya kawaida aliyoyafanya Rais Kikwete, hayakuwa ya kashfa
kutokana na ripoti ya CAG,” alisema na kuongeza.
“Ndio
maana leo hii nasimama kwa kujiamini mbele yenu, kama mtu anao ushahidi
ajitokeze aseme hadharani kuwa mimi niliondolewa katika Baraza la
Mawaziri kwa kashfa,” alisema.
Aja na vipaumbele vinne
Alisema
endapo atachaguliwa kuiongoza Tanzania, Serikali yake itakuwa na
vipaumbele vichache vinne vya kimkakati vitavyoiwezesha nchi iweze
kufanikiwa na kufikia malengo ya kuwa taifa lenye kipato cha kati.
Alivitaja
vipaumbele hivyo kuwa ni ujenzi wa uchumi imara, kuimarisha utawala
bora, kuboresha huduma za jamii (elimu, afya na maji) na kuimarisha
miundombinu ya usafirishaji ikiwemo ya reli, bandari, barabara sanjari
na kuiwezesha kuwa na umeme wa uhakika.
“Vipaumbele
vyangu vikuu ni vinne, kujenga Uchumi imara; kipaumbele namba mbili ni
Utawala Bora; kipaumbele namba tatu ni Huduma za Jamii (Elimu, Afya na
Maji); kipaumbele namba nne ni Miundombinu kama reli, bandari, barabara
na umeme wa uhakika,” alisema .(Muro)
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.