Chelsea itaanza utetezi wa taji la ligi ya Uingereza wakati itakapoikaribisha nyumbani Swansea katika wikiendi ya tarehe 8-9 mwezi Agosti.
Manchester City iliomaliza pointi nane nyuma ya Chelsea itaelekea West Bromwich huku Manchester United ikikabiliana na Tottenham katika uwanja wa Old Trafford.
Arsenal itaialika West Ham ,Liverpool ikienda Stoke,Newcastle itakabiliana na Southampton huku Leicester ikiialika Sunderland nyumbani.
Bournemouth iliopandishwa daraja,Watford na Norwich zitakabiliana na Aston Villa,Everton na Crystal Palace mtawalia.
Msimu huu utanza wiki moja mapema ikilinganishwa na msimu uliopita.CHANZO BBC SWAHILI
Chapisha Maoni