Kada
maarufu wa chama cha mapinduzi ambaye pia ni mfanyabiashara wa madini
jijini Arusha, Justine Nyari, akizungumza katika mkutano wa hadhara wa
kujinadi nafasi ya Ubunge kupitia chama cha mapinduzi katika kata mpya
ya Sinoni jijini Arusha(
Mkurugenzi
mtendaji wa kampuni ya Bushbucks Safaris iliyopo jijini Arusha, Mustafa
Panju akizungumza na wananchi wa kata mpya ya Sinoni kuhusu nia yake ya
kugombea nafasi ya Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi ambapo amewataka
wanaccm kudumisha mshikamano kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi ili
kupatikane ushindi wa kishindo.
Emmanuel Ole Njoro ambaye ni Mgombea nafasi ya Ubunge jimbo la Arusha mjini akijinadi katika kata ya Sinoni.
Thomas Munis mgombea Ubunge akijinadi kwa wananchi wa Sinoni.
Katibu
wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz Bano ambaye pia ni msimamizi wa
uchaguzi akitoa maelekezo kwa wananchi namna ya kuwasikiliza wagombea
ambapo aliwataka wasipige makofi wala kushangilia wakati wagombea hao
wakijinadi.
Kada
maarufu wa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni mfanyabiashara wa madini
jijini Arusha, Justine Nyari, anayeomba ridhaa ya CCM katika nafasi ya
ubunge ametangaza kuelekeza nguvu zake kwa vijana wasio na ajira kwa
kuwawezesha kujiajiri na kujipatia kipato
Aliyasema
hayo leo wakatia akizungumza katika kampeni ya kuwanadi wagomea Ubunge
wa Chama cha mapinduzi CCM, mkoani Arusha katika kata mpya Sinoni ,
uliohudhuriwa na wagombwa 12 wa nafasi ya Ubunge
Nyari
alisema kuwa changamoto kubwa inayoikabili Taifa kwa sasa ni pamoja na
ukosefu wa ajira kwa vijana na kuahidi kuwa endapo atachaguliwa kuwa
Mbunge wa jimbo la Arusha mjini atahakikisha vijana wanajiajiri wenyewe
Alisema
kuwa katika kusaidia hilo vijana watapewa elimu ya ujasiriamali na
baaade kujiajiri wenyewe hali itakayosaidia kukua kwa uchumi wa Taifa
letu na vijana kuongeza kipato chao
Akawataka
vijana kuacha kutumika kuleta vurugu na badala yake wawe wamoja katika
kuhakikisha wanaweza kujiletea maendeleo na si vingine kwani wao
wamekuwa wakitumika katika sehemu mbali mbali bila kupata manufaa
stahiki
“Nawaomba
vijana mujiandae kwa ajili ya kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira kwani
nimejipanga kuhakikisha mnapata elimu ya ujasiriamali ilimuweze
kujiletea maendeleo na kuongeza kipato chenu na pato la taifa”alisema
Nyari.
Kwa
upande wake Mustapher Panju anaeomba kupewa tiketi na CCM ya nafasi ya
ubunge aliwataka wagombea wenza katika kinyang’anyiro cha ubunge kupitia
ccm kudumisha upendo,mshikamano,na umoja miongoni mwao vitakavyosaidia
kukuza amani ndani ya chama na kuondosha makundi ambayo yamekuwa
yakikiangusha chama katika chaguzi zilizopita.
Alisema
kuwa changamoto za jimbo la Arusha anazijiwa hivyo wakimpa ridhaa ya
kupeperusha bendera ya CCM atahakikisha umoja,mshikamano na upendo
vinatawala ili wananchi waweze kujiletea maendeleo.
Panju
alisema kuwa atakapopitishwa na CCM kupeperusha bendera ya chama hicho
kwa nafasi ya ubunge atahakikisha kuwa anal eta maendeleo tarajiwa kwa
wakati kwani yeye atakuwa mtumishi wa wananchi wote bila kujali itikadi
za vyama.
Naye
Emmanuel Ole Njoro ameomba kupeperusha bendera ya CCM kwa nafasi ya
Ubunge ambapo alisea akipewa ridhaa atahakikisha kuwa anadumisha Amani
mshikamano na umoja miongoni mwa jamii huku akiandaa mipango ya
kuhakikisha vijana wanapata nafasi za kujifunza ujasiriamali ili waweze
kujiletea maendeleo.
Alisema
kuwa jografia ya jimbo la Arusha anaifahamu pamoja na changamoto zake
hivyo anaowaomba wanachama wa CCM kuhakikisha wanampatia nafasi ya
kupeperusha bendera ya chama hicho
Kwa
upande wake Thomas Munisi alisema kuwa tahakikisha changamoto
zinazowakabili wakazi wa jimbo la Arusha anazipatia ufumbuzi pindi
wanachama wa CCM watakapompatia ridhaa August 1
Alisema
kuwa fedha za miradizinazokusanywa na halmashauri hazitachakachuliwa na
zinaelekezwa katika miradi husika ilikuweza kulibadili jimbo la Arusha
kwani nia na uwezo wa kuwatumikia wakazi wa jiji la Arusha anao hivyo ni
wajibu kwa wagombea kuhakikisha wanakuwa wamoja,na mshikamano miongoni
mwao.
Chapisha Maoni