

KAMPUNI YA HUAWEI YAZINDUA NA SIMU MPYA YA
KISASA YA P8
-Itaanza kuuzwa nchini wiki hii
Johannesburg, Julai 3: 2015:Shamrashamra za kila aina zilitawala jana mjini Johanesburg nchini Afrika ya Kusini wakati kampuni ya Huawei ilipozindua simu mpya ya Smartphone ya kisasa aina ya P8 katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa klabu ya Country.
Mji
wa Johannesburg ni moja ya miji mikubwa ya utalii duniani miji mingine ikiwa ni
Bangkok,Singapore,Newyork na London ambako pia uzinduzi umefanyika ambapo
Meneja Mpya wa Bidhaa za wateja na Biashara ukanda wa Huawei Afrika ya
Kusini Charlene Munillal alizindua simu hii ya kisasa na kuonyesha
jinsi ilivyotengenezwa kwa kiwango cha juu cha ubunifu kwa kukidhi matumizi ya
aina mbalimbali katika soko.
Simu
hii itakuwa kwenye soko la Afrika na nchi nyinginezo kuanzia katikati ya mwezi
huu kwa Tanzania simu hii itaanza kupatikana katika soko la ndani ya muda wa
wiki moja kuanzia sasa kwa bei ya gharama nafuu na wateja 100 watakao agiza
simu hizi kupitia tovuti ya Huawei Tanzania kuanzia kesho watajishindia zawadi
mbalimbali zenye thamani ya shilingi 300,000/-
"Lengo
la kuleta simu hii ya Huawei P8 kwenye soko ni kuwawezesha
wateja wote duniani kupata simu ambayo ni ya kisasa na rahisi
kuitumia ikiwa inakidhi mahitaji mbalimbali na simu hii inathibitisha
dhmira ya kampuni yetu ya kuendelea kuingiza bidhaa bora za mawasiliano kwenye
soko”Amesema Charlene Munillal Meneja Mkuu wa Huawei Afrika ya Kusini
anayeshughulika na bidhaa na wateja.
Simu ya P8
yenye muundo wa kuvutia ambayo imetengenezwa kwa kiwango cha juu cha
kiteknolojia ambayo ni rahisi kwa mtu yeyote kuitumia ina mvuto wa pekee kwa
watumiaji na itaanza kuingia kwenye soko la Afrika ya Kusini katika wiki ya
pili ya mwezi huu.
Charlene
anasema simu ya P8 imetengenezwa kwa kutumia malighafi bora ikiwa na ganda la
nje lililotengenezwa kwa madini ya Alminium na inavutia kwa kila kwa mwonekano
na ina uimara wa hli ya juu bila kusahau kiwango kikubwa cha kiteknolojia
kinachomuwezesha mtumiaji kuitumia kwa matumizi ya aina mbalimbali.Ina urefu
wa mm6.4 na uzito wa gramu 144 na inapatikana katika rangi za aina
mbalimbali kulingana na mahitaji ya mteja ambazo ni Shaba,Dhahabu,Nyeusi na
kijivu.
Muundo wake
kuanzia mwonekano,ubunifu wa kiteknolojia uliotumika kuitengeneza na urahisi
wake kutumia kuweza kutumika kwa huduma za ziada kama vile kupiga picha na
video bora ni moja ya mambo yanayoifanya simu hii kuwa ya aina yake
na kuwa na sifa ya kipekee.
Programu ya
Android Lollipop 5.0 inayopatikana katika simu hii mpya inarahisisha
kuona,kutuma na kupokea ujumbe mfupi wa maneo hata wakati ambapo kioo cha simu
kinakuwa kimezimwa na kuna programu ya kuhifadhi kumbumbu za mtumiaji zisisomwe
na mtu asiyehusika nazo hata wakati ambapo simu inakuwa imepotea ama kuibiwa.Inazo
programmu nyingi za kisasa ambazo zinarahisisha kutafuta taarifa mbalimbali kwa
urahisi kwenye mtandao wa Google bila usumbufu wa aina yoyote.
Sifa nyingine
ya pekee katika simu hii mpya ya P8 ni kuwa na uwezo wa kuongezeka sauti kuwa
kubwa kwa kiwango cha asilimia 58 zaidi ya kiwango cha kawaida iwapo mtumiaji
anakuwa kwenye sehemu zenye kelele na kuwa rahisi kwake kuendelea kupata
mawasiliano na haina mawimbi endapo mtumiaji anaitumia kwa kutumia waya maalumu
wa kusikilizia simu masikioni au unapotumia kipaza sauti kimoja cha simu bila
kusahau kudumu na chaji ya betri kwa muda mrefu.
Pia simu hii
mpya mbalina kuwa na mambo mengi ya kisasa na yanayoleta furaha kwa mtumiaji
inaouwezo wa kuifadhi kiasi kikubwa cha kumbukumbu kufikia 16GB AU 64GB na ikiunganishwa
na interneti inakuwa na kasi ya ajabu katika kupakua data uwezo wake
ukiwa zaidi ya mara tatu ya uwezo wa simu zilizotengenezwa na makampuni
mengine zilizopo kwenye masoko hivi sasa na inao uwezo wa kudaka mawasiliano na
kusikika vizuri hata iwapo mtumiaji anasafiri kwa kutumia treni iendayo kasi
kwa mwendo wa Kilometa 300 kwa saa.
Mwisho
Kuhusu Kampuni ya
Huawei
Huawei ni kampuni
inayoongoza duniani kwa kuzalisha bidhaa za kurahisisha mawasiliano na
teknolojia na inarahisisha maisha kupitia ubunifu wa bidhaa bora za teknolojia
ya habari na mawasiliano kukidhi matakwa ya wateja wanaotumia simu na vifaa
vingine vya mawasiliano.
Huawei imeajiri
wafanyakazi wapatao 150,000 duniani kote ambao wanafanya kazi na makampuni ya
mawasiliano ya simu,wafanyabiashara wanaouza bidhaa za mawasiliano na
wateja wanaotumia bidhaa hizo.Huduma,bidhaa na ubunifu wa teknokojia ya
mawasiliano wa Huawei umesambaa katika nchi zaidi ya 170 duniani na inahudumia
zaidi ya moja ya tatu wa watu duniani.Ilianzishwa mwaka 1987 na ni
kampuni binafsi ambayo hisa zake zinamilikiwa na wafanyakazi wake.
Chapisha Maoni