Kiongozi wa Kundi Vijana wa 4U Movement, liliokuwa likimuunga mkono
Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, Hemed Ali akizungumza na waandishi
wa habari jjini Dar es Salaam leo Julai 18, 2015 kuhusu msimamo wao wa
kuungamkono UKAWA
Vijana wa Kundi la 4U Movement, liliokuwa likimuunga mkono Waziri
Mkuu wa zamani Edward Lowassa, washangilia baada kuzungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu msimamo wao wa kuungamkono
UKAWA.
KUNDI la vijana la 4U Movement, lililokuwa likimiuunga mkono Waziri
Mkuu wa zamani, Mh. Edward Lowassa, wakati wa mchakato wa kumpata
mgombea kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama
Cha Mapinduzi, CCM, limetangaza leo Jumamosi Julai 18, 2015, kuunga
mkono vuguvugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi, almaarufu kama UKAWA.
Tangazo hilo lilitolewa na Mratibu wa Taifa wa Kundi hilo, Hemed Ali,
wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es
Salaam mapema leo mchana.
Baadhi ya wanachama wa kundi hilo walikuwepo wakati kiongozi wao anatangaza msimamo huo mpya.
Sababu za kuunga mkono UKAWA, zimeelezwa na kiongozi huyo kuwa ni
kutoridhishwa na mwenendo wa mchakato wa kumpata mgombea wa CCM, ambapo
walidai kuwa katiba ya CCM haikufuatwa na baadhi ya makada wa chama
hicho, akiwemo Mh. Lowassa, hawakutendewa haki.
Chapisha Maoni