Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mwenyekiti wa Bodi
ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Ndugu Sabetha
Mwambenja mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu
Julius Nyerere. Maonesho hayo yalifunguliwa rasmi na Mheshimiwa Rais
Dkt. Jakaya Kikwete tarehe 3.7.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Ndugu Jacqueline
Maleko mara baada ya kuwasili kwenye sherehe za ufunguzi wa Maonesho ya
Sabasaba kwenye Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam tarehe 3.7.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Biashara wa TANTRADE, Ndugu Edwin Rutageruka wakati
alipowasili kwenye viwanja vya maonesho vya Mwalimu Julius Nyerere
kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa maonesho hayo uliofanya na Mheshimiwa
Rais Dkt. Jakaya Kikwete tarehe 3.5.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa na Mama Anna Mkapa
kutembelea banda la Taasisi yake ya Fursa Sawa kwa wote (EOTF) mara
baada ya Mheshimiwa Rais Dkt. Jakaya Kikwete kufungua rasmi maonesho
hayo tarehe 3.7.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiambatana na mwenyeji wake Mama
Anna Mkapa wakiangalia bidhaa mbalimbali za akina mama wajasiriamali
kutoka mikoa ya hapa nchini. Akina mama hao wanaratibiwa na Taasisi ya
Fursa Sawa kwa Wote inayoongozwa na Mama Anna Mkapa.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,
Mama Salma Kikwete akiwa na Mama Anna Mkapa wakifurahia bidhaa za vikapu
zilizotengenezwa na akina mama wajasiriamali kutoka mkoani Singida
kwenye Maonesho ya Sabasaba yanayofanyika Dar es Salaam
Chapisha Maoni