0
Mbinu ya kutoa uhai yatumiwa na madaktari Colombia

Mgonjwa mmoja wa saratani ya koo atolewa uhai hospitalini baada ya tiba kukosekana nchini Colombia

Kwa mara ya kwanza, madaktari nchini Colombia wametumia mbinu ya kutoa uhai kwa Ovido Gonzalez aliyekuwa akisumbuliwa na maradhi ya saratani ya koo.

Gonzalez mwenye umri wa miaka 79, alitolewa uhai katika hospitali moja ya mji wa Pereira baada ya kuhangaishwa kwa muda mrefu na maradhi hayo yasiyokuwa na tiba.

Mahakama kuu ya katiba nchini Colombia iliwahi kuidhinisha mbinu hiyo ya kutoa uhai mwaka 1997 ingawa haikupitishwa rasmi na kamati ya sheria.

Baadaye, mahakama kuu ikatoa ombi la kupitishwa kwa mbinu hiyo ambapo wizara ya afya iliunga mkono matumizi yake kwa masharti maalum yaliyobainishwa.

Gonzalez amekuwa mtu wa kwanza kutolewa uhai kisheria nchini Colombia ingawa mbinu hiyo inaarifiwa kutumika kwa muda mrefu kinyume na sheria.

Chapisha Maoni

 
Top