KLABU ya
Simba imefanya kweli tena baada ya leo kuzindua kadi mpya za uanachama
ambazo zitatoa fursa kwa watakaojiunga kunufaika na bima ya maisha.
Akizungumza
katika hafla ya uzinduzi wa kadi hizo jijini Dar es Salaam leo mchana,
Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva, amesema kila mwanachama atakayejiunga
na kuchukua kadi mpya, atapata bima ya maisha inayojulikana kwa jina la
'Simba Pamoja'.
Amesema
bima hiyo itampatia mwanachama ambaye amelipa malipo yake ya mwaka ya
uanachama fedha taslimu zisizopungua Sh. 250,000 ikiwa atapata msiba kwa
kufiwa na mtoto, mke ay yeye mwenyewe.
Aveva
amesema malipo ya uanachama hayajabadilika na yanaendelea kuwa Sh. 1,000
kwa mwezi, hivyo mwanachama atalipa ada ya mwaka Sh. 12,000 kwa
wanachama hai na Sh. 30,000 kwa wanachama wapya.
“Hii
ndiyo klabu pekee Afrika Mashariki na Kati inayotoa fao hili kwa
wanachama wake, Simba inajali sana wanachama wake na tutaendelea
kuimarisha uhusiano wa klabu na wanachama,” amesema Aveva.
Aveva
ambaye alikuwa amefuatana na makamu wake, Geofrey Nyange 'Kaburu' pamoja
na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa kampuni ya EAG Group, Imani Kajula, pia
amezindua kadi ya Simba kwa ajili ya watoto wanaoipenda timu hiyo
'Simba Cub Membership Card' ili kuwawezesha kutambuliwa na kuwa
wanachama wa timu hiyo.
“Kadi ya
Simba Cubs itawawezesha watoto siyo tu kutambuliwa kuwa wanachama wa
Simba, bali kupata punguzo kubwa au kuingia bure kwenye matukio
yanayoandaliwa na Simba na kwenye maduka (yanayouza bidhaa za Simba) pia
yatatoa punguzo kwa watoto wenye kadi hizo,” amesema.
Kajuna
amesema upatikanaji wa kadi hizo ni moja ya majukumu ya kampuni yao
waliyoingia na klabu ya Simba kuhakikisha wanabuni mbinu zitakazoisaidia
klabu hiyo kupata mapato.
Chapisha Maoni