Timu
ya taifa ya wanawake ya England imetupwa nje ya michuano ya kombe la
dunia la wanawake kwenye mchezo wa nusu fainali kwa kichapo cha goli 2-1
kutoka kwa Japan ambao ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo kwenye
michuano inayoendelea huko nchini Canada.
Japani
walikuwa wakwanza kupata goli la kwanza dakika ya 33 kupitia kwa nahodha
wao Aya Miyama baada ya Claire Rafferty kumfanyia madhambi Saori
Ariyoshi nje kidogo ya eneo la hatari lakini mwamuzi akaamuru ipigwe
penati na Miyami akaukwamisha mpira kambani.
Dakika saba baadaye, England walisawazisha goli hilo kwa mkwaju wa penati pia kupitia kwa Fara Williams aliyefunga penati hiyo.
Goli la
kujifunga la Laura Bassett dakika za majeruhi liliwapa ushindi Japan na
kuwapeleka kwenye hatua ya fainali ambako watakutana na timu ya taifa ya
Marekani.
Chapisha Maoni