BAADA ya
vuta nikuvute ya wazazi wa wanafunzi, Hilary na Hamis ‘watoto wa
Diamond’ walioshinda katika shindano la kucheza Ngololo mwaka jana na
staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuahidi kuwasomesha
katika shule ya East Africa International iliyopo Mikocheni, Dar huku
akishindwa kuwalipia ada na watoto hao kurudishwa nyumbani, hatimaye
wamerejeshwa tena shuleni.
Ilidaiwa
kwamba wamewakataza kuzungumza kwenye vyombo vya habari kutokana na
kwamba walichukizwa na habari hiyo kuvuja na kuripotiwa na gazeti hili
kwa mara ya kwanza.
“Wale
watoto wamerudi shule tayari baada ya kukaa nyumbani kwa miezi kadhaa,
naamini hata gazeti lenu lilisaidia sana kuwashtua kwani vinginevyo
wasingerudi na ndiyo maana hata wazazi waliambiwa wasiongee na ninyi,”
kilisema chanzo hicho.
Naye
mmoja wa wazazi wa watoto hao kwa sharti la kutokutajwa alisema: “Kwa
sasa niko safarini ila ni kweli watoto wamerudi shule ila mambo bado
hayajawa mazuri sana, sema ndiyo wako kwenye mazungumzo zaidi na suala
hilo nimewakabidhi ndugu zangu ambao wako eneo la tukio ili
walishughulikie.”
Chapisha Maoni