
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo ameeleza msichana
huyo alimnyonga mtoto huyo baada siku ya jumatano baada ya kutokea
mabishano kati ya marehemu na mtuhumiwa marehemu akimtuhumu dada yake
kumuibia sox za shule huku akimlushia maneno ya kejeli ndipo mtuhumiwa
akachukua uamuzi wa kumsukuma marehemu ambapo baada ya marehemu
kudondoka sakafuni mtuhumiwa alimbeba kumpeleka chumbani na kumnyonga
kwa kutumia kamba ya gauni na kusababishia kifo chake.
Nao wakazi wa mji wa Morogoro wakizungumzia tukio hilo wametupia
lawama baadhi ya wazazi kuwanyanyasa ndugu zao ambapo wamesema wazazi na
walezi wanawajibu wa kuhakikisha wanawalea watoto kwa kuzingatia haki
sawa ili kuepusha mauaji na unyanyasaji usiokuwa wa lazima.
Chapisha Maoni