
Wakala wa maandalizi ya Harusi mjini
Moscow wamewakodishia magari ya kivita( Deraya) maharusi wapya ili
yawasindikize kwenda kwenye sherehe yao badala ya kukodi gari ya
kifahari aina ya limo kwa madai kuwa hayaleti shamrashamra katika
sherehe.
Meneja wa wakala hao ameiambia Televisheni ya Urusi, NTV kuwa kila kitu hutegemea usajili,Kama wewe usajili wako ni kuendesha gari kando ya Barabara ya Moscow au katikati basi gharama zinatofautiana;kodi ya gari ya Deraya itakuwa ghali zaidi, na kama unataka kutumia pesa kidogo basi inabidi kuepuka kutumia barabara za katikati ya jiji kabisa na kutoka nje kidogo. Afisa wa polisi aliiambia Redio ya Ekho Moskvy kwamba kazi ya magari ya Deraya ni kuchukua vifaa vikubwa na kwa hiyo kuna haja ya ruhusa maalum kutoka mamlaka husika na uratibu wa Polisi.
Chapisha Maoni