
Watu sita wamewekwa karantini
gerezani nchini Guinea baada ya kushutumiwa kusafiri wakiwa na mwili wa
mtu aliyekufa kwa ugonjwa wa Ebola.
ikiwa baada ya siku 21 hawataonyesha dalili yeyote ya kuwa na Virusi vya Ebola watafikishwa mahakamanni kwa makosa ya kukiuka sheria za maswala ya afya.
Guinea iko kwenye Kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa Ebola.
Takriban watu 2,500 wamepoteza maisha nchini Guinea tangu ugonjwa huo ulipokumba Afrika Magharibi zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Chapisha Maoni