
Askari mmoja ameripotiwa kujeruhiwa
baada ya kuwepo kwa mapambano makali kati ya Polisi na Wanamgambo wa Al
Shabaab Kaskazini Mashariki mwa Kenya
Viongozi katika eneo hilo wamesema Magari manne ya Polisi yamechomwa moto na wanamgambo. Polisi wameiambia BBC kuwa wamepeleka kikosi kuimarisha hali ya usalama.
Taarifa za awali zilieleza kuwa askari kadhaa wanahofiwa kufa kwenye kwenye shambulio la usiku wa jumatatu.
Wakati huo huo al shabaab wamedai kuhusika katika shambulio hilo wakidai kuwa wamewaua Polisi 20, lakini vyombo vya usalama vimesema madai hayo ni Propaganda. Siku ya jumatatu Polisi watatu walijeruhiwa baada ya Gari lao kukanyaga Bomu la kutegwa ardhini.
Kikosi cha askari 20 kilifika katika eneo hilo kuwasaidia waliojeruhiwa wanaoelezwa kushambuliwa na Al Shabaab. Al shabaab wamekiri kuhusika katika shambulio hilo na kuchoma magari mjini Garissa.Msemaji wa kundi hilo Shaykh Abdiasis Abu Mus’ab amesema shambulio hilo limefanywa na kikosi maalum kiitwacho ‘mujahidin’.
Mus’ab amesema shambulio lilikuwa la “mafanikio” na kudai kuwa hasara waliyoipata askari wa Kenya ni kubwa.
Chapisha Maoni