Wanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Iringa wakiwa katika mgomo leo kutokana na
kutopata mkopo kwa wakati ambapo inapelekea kushindwa kabisa kuendesha
maisha yao chuoni hapo baada ya serikali kupitia bodi ya mikopo
kuwacheleweshea pesa zao.
Viongozi
wa serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa wakiwatuliza
wenzao leo baada ya mgomo wa wanachuo wa chuo cha UoI kugoma
wakishinikiza kupewa mikopo yao ili kuendesha maisha chuoni hapo.
Mkuu
wa chuo kikuu ya Iringa Prof Joshua Madumulla akizungumza na wanafunzi
hao baada ya kutokea mgomo chuoni hapo leo asubuhi.
Mmoja
wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Iringa akitoa malalamiko yake dhidi
ya bodi ya mikopo kwa kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Angeline Mabula
leo kuhusu kucheleweshewa mikopo yao.
Kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Mabula akizungumza na wanafunzi hao wakati wa mgomo wa wananchuo wa chuo cha Iringa leo
Ulinzi ulikuwa ni wakutosha chuoni hapo
Chapisha Maoni