WANAFUNZI wa vyuo vikuu vya UDOM, Mkoani Dodoma na kile cha DUCE
jijini Dar es Salaam, waliamua kuacha masomo na kugoma kushinikiza bodi
ya mikopo kulipa mikopo yao. Mgomo huo unakuja siku mbili tu baada ya
wenzao wa UDSM kugoma kwa madai kama hayo na hatimaye siku iliyofuatia
wakalipwa. Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alilazimika kumtuma naibu waziri
wa Afya Steven Kebwe na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa ili
kutuliza "mzuka" wa wanafunzi ambapo baadhi yao walilia kwa uchunghu
kama Eva Joseph, ambaye naibu waziri alilazimika kufanya kazi ya ziada
kumtuliza na kumbebeleza. Pichani juu ni wanafunbzi hao wa UDOM,
wakionyesha bango
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa akihutubia wanafunzi hao ambao walikuwa watulivu wakati wote wa mgomo
Chapisha Maoni