Akizungumza na vyombo vya habari mchana huu DKt.Likwelile ambaye ni
amemuwakilisha Waziri wa Fedha na katika Mkutano wa Benki ya Dunia
amesema kuwa,”Mkurungezi wa Kanda ametoa ripoti ya mwaka, ameelezea ni
namna gani ukanda huu wa Afrika ulivyokuwa ukifanya kazi za maendeleo,
ameelezea ripoti hiyo kuwa inagusa nchi zote sita za Afrika. Nchi hizo
ni pamoja na Rwanda, Tanzania,Uganda, Kenya, Ethiophia na Visiwa vya
Shelisheli, Aidha nchi hizo zimefanya kazi vizuri. Alisisitiza
Likwelile.
Likwelile amefanafua kuwa, “Mkurugenzi wa ukanda wanchi za Afrika
ameelezea jinsi uchumi unavyokua kwa kasi kubwa kwani umekua kwa
asilimia sita mpaka saba na ukuaji huu wa uchumi unawanufaisha watu wote
wa nchi hizo.
Ni Muhimu kuwekeza kwenye reli hii itawapunguzia wananchi usumbufu
wanaoupata kwenye masuala ya usafiri na usafirishaji wa mizigo.Aliongeza
Likwelile.
Pia Likwelile amezungumzia kuhusu kuendeleza kilimo hasa kilimo
chenye tija. alisema kuwa kilimo cha biashara humuongezea kipato
mwananchi wa chini na kumfanya kujikwamua kwenye hali ya kimasikini.
Aidha mwenyikiti amezungumzia suala nishati hasa nishati ya umeme ili
tuweze kuendelea ni muhimu kusimamia suala la umeme kwa kikanda. Hii
itapelekea nchi zote za Afrika kunufaika na masuala ya maendeleo
kiujumla kwa nchi hizo za kikanda.
“ Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu wa rais, Aidha ukanda wa nchi
za Afrika unapenda kumshukuru raisi aliyepita Dkt. Kaberuka kwa kazi
nzuri aliyoifanya kwani ameziacha nchi katika hali nzuri sana”
Alisisitiza Likwelile
Mwisho Likwelile alifafanua kuwa, “Benki ya Maendeleo ya Afrika
imetambua umuhimu wa kazi na mchango mkubwa alioutoa Mhe. Jakaya Mrisho
Kikwete na ndio maana imemualika katika Mkutano huu wa mwaka kutokana na
kazi zuri aliyoifanya.
Imetolewa na Msemaji wa
Wizara ya Fedha
Ingiahedi C. Mduma
ABIDJAN
25 MEI 2015.
Chapisha Maoni