0

Mgogoro wa ardhi kati ya wakazi wa tarafa ya Loliondo serikali na mwekezaji kugombea eneo la kilometa za mraba elfu moja na mia tano umeanza kuibuka upya baada ya wananchi kudai serikali imeanza mchakato wa kulichukua eneo ilo na kuwataka waondoke wakati waziri mkuu alishamaliza mgogoro huo huku baadhi ya watetezi wa haki za wafugaji wakidai kutumiwa jumbe za vitisho na watu wasiyo julikana.
Wakizunguzia hatua ya kuibuka upya kwa mgogoro huo watetezi wa haki za wafugaji kutoka mashirika yanayo jihusha na utetezi wamesema kimsingi waziri mkuu Mizengo Pinda alishamaliza mgogoro huo mwaka jana alipotembelea eneo ilo na kuruhusu shughuli za kifugaji kuendelea sambamba na uhifadhi lakini hali imeanza kubadilika na kutishiwa maisha kinyume na maamuzi ya waziri mkuu.
Mratibu wa mtandao wa wafugaji Tanzania Joseph Parsambey amesema hatua hiyo ina lengo la kuwaumiza zaidi ya wakazi elfu themanini wanao ishi katika vijiji nane vinavyo zunguka pori la akiba la Loliondo kwa mgongo wa mapito ya wanyamapori huku lengo likiwa ni kuwapati wawekezaji kutoka nje ya nchi na kuwa acha watanzania bila matumaini huku wanawake nao wakilalamikia kuteseka kwa matukio yanayo jirudia na kuitaka serikali iwe na msimamo kwani wanawake wa Loliondo kamwe hawataondoka katika ardhi yao.
Mnamo tarehe ishirini na tatu mwezi wa tisa mwaka jana (2013) waziri mkuu  Mhe Mizengo Pinda alifanya ziara katika eneo lenye mgogoro kutembelea vijiji vyote na kutoa maamuzi ya serikali kuwa imeamua wakazi hao waendelee kuishi kama ilivyokuwa mwanzo maamuzi ambayo yanatajwa kukiokwa bila taarifa kwa wananchi amba sasa wanatakiwa kuondoka katika eneo ilo.

Chapisha Maoni

 
Top