0

Rais wa Afrika  kusini Jacob Zuma  anametaka uchaguzi wa urais nchini Burundi kuahirishwa.

Zuma amesema hayo baada ya mkutano wa kieneo nchini Angola, kuwa uchaguzi huo haupaswi kufanyika hadi hali ya amani itakaporudi nchini humo ambapo maandamano  bado yanaendelea hususan katika mji wa Bujumbura kufuatia jaribio la mapinduzi la wiki iliopita.

Wafanyikazi wa mahospitali nchini Burundi awali walielezea kuwa kumekuwa na mshambulizi ya kulipiza kisasi ambapo polisi wamekuwa wakiwajeruhi wanajeshi waliodaiwa kuhusika na jaribio hilo lakini Rais wa taifa hilo Bwana Pierre Nkurunziza amekana madai ya kutaka kulipiza kisasi dhidi ya watekelezaji wa shambulio hilo.

Chapisha Maoni

 
Top