
Ripoti za mahakama nchini Burkina
Faso zinasema kuwa mwili ambao unakisiwa kuwa wa raisi wa zamani
aliyeuawa Thomas Sankara utafukuliwa hii leo katika jaribio la kutaka
kubainisha ikiwa ni wake.
Bwana Sankara aliuawa wakati wa mapinduzi mwaka 1987. Sankara alichukuwa uongozi baada ya mapinduzi ya mwaka wa 1983.
Sankara alipinduliwa na Blaise Compaore ambaye aliitawala Burkina Faso hadi mwaka uliopita alipolazimishwa kuondoka na maandamano makubwa katika mji mkuu wa wa nchi hiyo Ouagadougou.
Madaktari wawili kutoka Burkina Faso na mmoja kutoka Ufaransa watachukua chembechembe za mwili huo na kuipima wakitumia mashine na mbinu za kisasa za DNA ilikubaini kikamilifu iwapo inahusiana na mwili wa Sankara.
Miili mingine 12 ya wafuasi wake waliouawa pamoja naye pia itafukuliwa.
Mabaki hayo ya Sankara yamezikwa katika makaburi ya Dagnoen katika mji mkuu wa Ouagadougou.
Familia yake inashuku kuwa huenda mwili huo sio wake.

Chapisha Maoni