
Wizara ya Mambo ya nje Tanzania
imetoa taarifa juu ya kuwepo kwa mkutano wa Viongozi wa Afrika Mashariki
jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili ili kuangalia kwa mara nyingine
tena hali ya amani nchini Burundi.
Mkutano huu unaotarajiwa kufanyika karibuni haujaweka wazi kama Raisi huyo wa Burundi atakuwepo ila umeweka bayana kuwa Burundi itawakilishwa vyema. Upinzani nao nchini humo umegoma kufanya mazungumzo baada ya mmoja wa viongozi wake kuuwawa siku ya Jumamosi.
Machafuko ya sasa yamesababisha zaidi ya Raia 100,000 wa Burundi kukimbilia nchi za jirani Rwanda, Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Chapisha Maoni