
Waziri mkuu nchini Ireland Enda
Kenny amesema kuwa Ireland ni nchi ndogo iliyo na ujumbe mkubwa baada ya
kupiga kura kwa wingi kuhalalisha ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
Kanisa katoliki lilifanya kampeni ya kupinga kura hiyo. Lakini Askofu mkuu wa mji wa Dublin Diarmuid Martin alikubali kushindwa na kusema kuwa matokeo hayo ni ishara ya mabadiliko ya kijamii nchini Ireland.
Wale waliokuwa wakiunga mkono ndoa za wapenzi wa jinsia moja waliitaja siku ya jana kuwa ya kihistoria nchini Ireland.

Chapisha Maoni