
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Said Mecki Sadiki
Rais
wa Msumbiji Mhe.Filipe Jacinto Nyusi anatarajia kuwasili nchini
Tanzania kesho Mei 17 kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ambapo pamoja
na mambo mengine atalihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma.
Akitoa
taarifa ya ziara hiyo leo jijini Dar es salaam Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam Said Mecki Sadiki amesema kuwa Rais Filipe Nyusi atawasili katika
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es
slaam, Mei 17,2015 majira ya saa 6 ambapo mara baada ya kuwasili uwanjani hapo, atalakiwa na viongozi
mbalimbali wa Serikali, kupata mapokezi ya burudani ya ngoma za asili na
kukagua gwaride la heshima litakaloandaliwa na Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzanian(JWTZ) na baadaye kupigiwa mizinga 21.(P.T)
Mhe.Sadiki
ameongeza kuwa mara baada ya mapokezi ya Rais huyo uwanja wa
ndege ataelekea Ikulu ambako atapokelewa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete na baadaye viongozi
hao wawili watakua na mazungumzo ya faragha.
Amesema
Mei 18, 2015 Rais Filipe Nyusi atafanya mazungumzo na wafanyabiashara wa
Msumbiji waishio nchini Tanzania na kisha kuendelea na ziara yake
Visiwani Zanzibar ambako atakutana na kufanya mazungumzo na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein.
Pia Sadiki ameeleza
kuwa baada ya kukamilisha ziara yake kisiwani Zanzibar Mei, 19, Rais Filipe ataelekea mjini Dodoma yalipo
Makao Makuu CCM ambako atakutana na
Mwenyekiti wa Chama hicho Rais Jakaya Mrisho Kikwete kabla ya kuelekea Ukumbi wa Bunge
kulihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumaliza ziara yake kabla ya kurejea nchini kwake.
Sadiki anaomba radhi kwa Wananchi wote hususan wakazi wa jiji la Dar es salaam
kuwa wavumilivu kutokana na usumbufu utakaotokana na baadhi ya barabara
zikiwemo Nyerere, mzunguko wa Kamata, Barabara ya Sokoine ,Luthuli na
Barabara ya Kilwa kufungwa mara kwa mara kupisha msafara wa kiongozi
huyo.
Chapisha Maoni