
Afrika
Kusini imeanzisha operesheni ya kuwafurisha raia zaidi ya 400 kutoka Msumbiji kurudi makwao kufuatia vurumai ya kibaguzi dhidi ya wageni
katika miji ya Durban na Johannesburg baada ya wenyeji kuanza kuwavamia wageni pamoja na kuwapora mali zao jambo lililopelekea watu saba raia wa kigeni kuuawa na wenyeji waliokuwa
wakilalama kuwa wageni hao wamechukua nafasi zao za kazi.
Serikali
ya Msumbiji imeshangazwa na hatua hiyo ya kuwaondoa raia wake kwa nguvu
huku waziri wake wa maswala ya kigeni Oldemiro Baloi akisema alikuwa
anatarajia kufanya mazungumzo na mwenzake wa Afrika Kusini Baloi huyo ameongeza kuwa haelewi kwa nini raia wa Msumbiji wanakamatwa na kuondolewa
nchini humo kwa nguvu ilihali swala hilo lilikuwa linashughulikiwa baina
ya serikali hizo mbili.
BBC imesema hatua hii ya serikali
imewashangaza wengi hususan baada ya serikali kupewa ilani ya mahakama
dhidi ya kuwakamata na kuwafukuza wageni. ambapo ''Operesheni Fiela'' ya kuwakamata wageni imekuwa ikiendeshwa majira ya alfajiri hasa
katika mitaa duni ya miji ya Durban na Johannesburg.
''Operesheni Fiela'' kama inavyofahamika imepelekea watu zaidi ya 889 kukamatwa na Wanaharakati
wa haki za kibinadamu wamekwenda mahakamani kupinga operesheni Fiela
wakisema inahalalisha vita vya kibaguzi vilivyo sababisha vifo vya watu
saba wengi wao wakiwa raia wa mataifa ya Afrika.CHANZO:BBC (Muro)
Chapisha Maoni