
Na Brighton Masalu-GPL
Msanii
Vincent Kigosi ‘Ray’ amekiri kwamba kufariki kwa Steven Kanumba
kumemsababishia kuporomoka kisanaa na kiuchumi kwa kukosa ushindani
thabiti kwenye game.(P.T)

Msanii Vincent Kigosi ‘Ray’.
Akizungumza
na mwandishi wetu katika mahojiano maalum hivi karibuni, Ray alisema
Kanumba alipokuwa hai, alikuwa na changamoto kubwa katika ubunifu wa
kazi na hata ushindani wa maisha ya kawaida.
Akatolea
mfano baadhi ya mambo yaliyokuwa yaking’arisha nyota yake kuwa ni pamoja
na kushindana katika kumiliki vitu kama magari, silaha binafsi
(bastola) na filamu zenye ubora, kitu ambacho kwa sasa haumizi kichwa
baada ya kuondoka kwa Kanumba.
Marehemu Steven Kanumba enzi za uhai wake.
“Kila
kitu kinapokosa ushindani maana yake kinapoa, kuondoka kwa Kanumba
limekuwa pigo kubwa sana kwangu kwani sina tena mtu wa kunipa changamoto
kama kipindi kile, ni kama nyota yangu imefifia,” alihitimisha Ray.
Chapisha Maoni