Mwenyekiti
wa chama cha Tnzania Labour Part (TLP) Agustino Mrema akizungumza na
waandishi wa Habari (hawapo) katika mkutano uiliofanyika kwenye ukumbi
wa Idara ya Habari MELEZO kuhusu kukanusha kuwa yeye amefukuzwa
TLP,Kushoto Mkurugenzi wa Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo,Kulia ni
Katibu Mkuu wa TLP,Nancy Mrikariya.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
MWENYEKITI wa Chama cha Tnzania Labour Party (TLP) Agustino Mrema,amesema hajafukuzwa unachama katika chama hicho.
Mrema
aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana kuwa yeye ni mwenyekiti wa
Chama hicho na hakuna mtu wa kumtoa kutokana na kuendesha chama hicho
kwa kufuata katiba.
Amesema
kikundi kinachofanya hivyo na kusambaza taarifa kuwa kimemtoa kutokana
na kufanya vikao hakitambui na kuwataka wanachama kuwabeza watu hao.
Mrema
amesema yeye akiwa Mwenyekiti ataendelea kutetea jimbo lake la
Vunjo,hivyo watu wanaosema amefukuzwa katika chama wapuuzwe. Aidha
amesema biashara ya Urais ameachana nayo ,sasa kazi yake ni Ubunge
kupitia jimbo la Vunjo na ameweza kuleta maendeleo ya wananachi katika
jimbo hilo.(Muro)
Chapisha Maoni