
Serikali imeahidi kumchukulia Shilole kufuatia kusambaa kwa picha zake chafu zilizopigwa wakati akitumbuiza nchini Ubelgiji.
Akizungumza
bungeni Dodoma jana, Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na
Michezo, Juma Mkamia, wakati akijibu hoja za wabunge baada ya kusoma
makadirio na matumizi wa wizara hiyo, alisema tayari serikali
imeliagiza baraza la sanaa taifa BASATA kufanya naye mahojiano.

Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Mkamia
“Tumemtaka
ajieleze kupitia BASATA, akishajieleza serikali itachukua hatua na
niombe mheshimiwa spika kupitia bunge lako tufuku, kuliomba radhi kwa
upande wa serikali kwa kitendo kilichofanywa na mwanamuziki yule. Sio
maadili yetu na nimesema akishajieleza serikali itachukua hatua yake,”
alisema Juma Mkamia.
Chapisha Maoni