
Afisa
Elimu Mkuu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bi Madina Juma,
akihutubia wakati wa maadhimisho ya siku ya hedhi duniani yaliyofanyika
kwa mara ya kwanza Tanzania jana jijini Dar es Salaam katika viwanja
vya mnazi mmoja. Kauli Mbiu ya mwaka huu inaeleza “Usisite kuzungumzia
hedhi”.


Wanafunzi
kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari jijini Dar es Salaam
wakiwa kwenye maandamano ya kuadhimisha siku ya hedhi duniani
yaliyofanyika kwa mara ya kwanza Tanzania jana jijini Dar es
Salaam.Kauli Mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inaeleza “Usisite
kuzungumzia hedhi”
Na Mwandishi Wetu
Tanzania
imeadhimisha siku ya hedhi duniani, ambapo wizara ya elimu kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali wamekubaliana kuandaa na kusimamia sera
inayoondoa vikwazo kwa watoto wa kike katika masomo yao.
Akizungumza
katika maadhimisho hayo jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Elimu Mkuu wa
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Madina Kemilembe, alisema
kukosekana kwa miundombinu rafiki mashuleni kunasababisha wanafunzi
kutohudhuria masomo.
Alisema
ukosefu wa mazingira bora kama vyoo, maji safi na salama pamoja na
vyumba mahsusi vya kubadilishia nguo , hasa kwa watoto wa kike wanapokua
katika hedhi mashuleni kunachangia utoro.
“Nawashukuru
wadau Water Aid, Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV), Kasole Secrets
pamoja na wengine kwa kuisaidia serikali kuandaa mazingira rafiki kwa
watoto wetu kwa kuwajengea vyumba vya kubadilishia na kuhakikisha
upatikanaji wa pedi kwa baadhi ya shule,” alisema Kemilembe.
Alisisitiza
juu ya utoaji wa elimu kwa wazazi na wanafunzi wa jinsia zote ili
kuondoa unyanyapaa ili kuboresha mazingira ya kusoma kwa mtoto wa kike.
Naye
Mkurugenzi wa Water Aid, Ibrahim Kabole, alisema kuna uelewa mdogo
pamoja na mila potofu zinazofanya jambo la hedhi kuonekana ni la aibu.
Chapisha Maoni