0
Shirika la umeme Tanzania Tanesco katika kukabiliana na changamoto ya vitendea kazi limezindua magari ya kazi 132 yenye thamani ya shilingi bilioni nane pesa za kitanzania ambayo yamesambazwa katika  wilaya zote nchini ikiwemo mikoa ya Mtwara na Lindi iliyokuwa na tatizo hilo.

Hafla fupi ya uzinduzi wa magari hayo kitaifa umefanyika mkoani Mtwara huku mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Felchesmi Mramba akisema magari hayo ni mapya yatasaidia kuboresha utendaji kazi na kuleta ufanisi hasa wilayani, huku akisisitiza shirika hilo kuendelea kujiboresha ili kuondoa malalamiko dhidi ya wananchi.
 
Akizungumzia uboreshaji wa kituo cha Mtwara na Lindi ambacho kinazalisha mega wati 18 ambazo haziendani na uwekezaji uliyopo hivi sasa anasema
 
Kwa upande wake meneja wa Tanesco mkoa wa Mtwara Azizi Salumu anazungumzia ujio wa magari hayo.

Chapisha Maoni

 
Top