Waziri
wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akiwa amebeba ndoo ya
maji kichwani alipokuwa akikabidhiwa visima 33 vilivyochimbwa kwa
msaada wa Watu wa Falme za Kiarabu na Balozi wa Falme hizo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akifungua bomba la maji
kuashiria uzinduzi wa mradi mkubwa wa maji katika Kata ya Olosokwani,
Loliondo wilayani Ngorongoro, juzi. Mradi huo umefadhiliwa na Serikali
ya Falme za Kiarabu (UAE) ambayo imewekeza wilayani humo. Uzinduzi huo
pia ulihudhuriwa na Balozi wa UAE nchini Tanzania, Mbarouk Nassor
Mbarouk.
WAZIRI
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akijindaa kumtwisha ndoo ya
maji mkazi wa Kata ya Olosokwani, ambako alizindua mradi mkubwa wa maji
ya visima virefu wilayani Ngorongoro, juzi. Anayeshuhudia ni Mkuu wa
Wilaya ya Ngorongoro,Hashimu Shaibu.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akifurahia uzinduzi wa mradi wa maji na wakazi wa
kijiji Olosokwani,
wilayani Ngorongoro juzi. Kushoto ni Balozi wa Falme za Kiarabu nchini
Tanzania, Mbarouk Nassor Mbarouk.
Chapisha Maoni