0
‘’Afrika inapaswa kuhusika na ukuzaji wa raslimali zake’’

Rais wa Afrika Kusini ahimiza nchi za Afrika kudhibiti na kuzikuza raslimali zake za madini

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, alitoa maelezo katika mkutano wa AU siku ya Ijumaa na kuhimiza nchi za Afrika kujihuisha na ukuzaji wa raslimali zake za madini badala ya kutegemea wawekezaji kutoka nchi za kigeni.

Zuma alisema, ‘’Tumekubaliana kama viongozi kwamba hatutoruhusu raslimali zetu za madini tunazozimiliki kukuzwa nje ya bara la Afrika. Shughuli zote za utengenezaji na ukuzaji zinapaswa kufanyika ndani ya Afrika ili kuweza kuwafaidisha watu wetu wa Afrika.’’

Wakati huo huo, Zuma pia alishiriki mashindano ya AU Presidential Golf Challenge yaliyolenga kuchangisha fedha kwa ajili ya miradi ya AU.

Zuma alitoa shukrani kubwa kwa wajumbe waliohudhuria mkutano wa AU na kudhihirisha furaha yake aliyokuwa nayo kwa kupata fursa ya kuandaa mkutano huo muhimu nchini Afrika Kusini. CHANZO TRT SWAHILI

Chapisha Maoni

 
Top