0
Muungano wa upinzani waundwa nchini Uganda

Vyama vya upinzani nchini Uganda vyaungana kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2016

Vyama vya upinzani vimeunda muungano kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2016 ili kumuondoa Rais Yoweri Museveni aliyekaa madarakani kwa miaka 30 nchini Uganda.
Muungano huo uliotambulishwa kwa jina la Democratic Alliance, unajumuisha vyama vya upinzani, makundi mbalimbali ya kisiasa pamoja na viongozi wa kijamii na kidini nchini Uganda.
Wawakilishi wa muungano huo walitia saini mkataba wa makubaliano tarehe 10 mwezi Juni, utakaotoa mwongozo katika uteuzi wa mgombea urais.
Waziri Mkuu wa zamani wa Uganda Amama Mbabazi, ambaye hakuhudhuria mkutano wa kutia saini mkataba wa makubaliano, anaonekana kuwa mgombea atakayeleta upinzani mkubwa kwa Museveni katika uchaguzi.
Makamu wa rais wa zamani Gilbert Bukenya pia amabaye amejitenga na rais Museveni, pia ni mmoja wa viongozi wakuu wa muungano huo.
Hata hivyo, hii sio mara ya kwanza kwa upinzani kuunda muungano dhidi ya chama tawala cha Museveni. Hapo awali, vyama vya upinzani viliwahi kuunda muungano katika uchaguzi wa mwaka 1996 na 2011 na kushindwa kumpiku Museveni huku wakidai kwamba uchaguzi haukufanyika kwa haki.

Chapisha Maoni

 
Top