
Askari 3 wauawa kwa bomu lililotegwa kando ya barabara na kundi la kigaidi Somalia
Kwa taarifa iliyotolewa na afisa wa kijeshi, Wanamgambo wa kiislamu nchini Somalia wametega bomu kando ya barabara, lililoua askari takriban 3 waliokuwa katika gari la kijeshi kusini magharibi mwa mji mkuu Mogadishu siku ya Jumanne.
Kikundi cha Kiislamu cha Al Shabaab, ambacho kinataka kuipindua serikali ya somalia, kimekuwa kikishambulia viongozi wa siasa, askari na wanasiasa katika taifa la Afrika ambalo linajijenga upya baada ya miaka mingi ya machafuko na migogoro.
Kapteni Farah Nur aliiambia reuters"Bomu hilo lililolipuka kando ya barabara ,mpaka sasa ni wanajeshi 3 wanaojulikana ndio waliokufa.
Aliongeza kusema kuwa shamblio hilo lilitokea katika kijiji cha Hawaabdi, kilichopo kilometa 17 km kusini magharibi mwa Mogadishu. CHANZO TRT SWAHILI
Chapisha Maoni