Kiongozi wa kund la Al-Qaeda nchini Yemen Nasir al-Wuhayshi auawa kwenye operesheni ya Marekani
Nasir al-Wuhayshi ambaye ni kiongozi wa kundi la Al-Qaeda nchini Yemen, ameripotiwa kuuawa kwenye mashambulizi ya angani yaliyotekelezwa na ndege zinazomilikiwa na jeshi la Marekani.
Mmoja wa viongozi wa Al-Qaeda Halid Batrafi, alisambaza picha kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter na kutangaza kuuawa kwa Wuhaish pamoja na rafiki zake wawili kwenye mashambulizi yaliyotekelezwa na Marekani.
Batrafi pia alielezea kwamba viongozi wa kundi la Al-Qaeda walikusanyika na kumteua Kasim al-Rimi kuwa kama kiongozi mpya aliyekubali kula kiapo cha kuziba pengo hilo.
Nasir al-Wuhayshi, ambaye aliwahi kuwa msaidizi wa Osama bin Laden, alitoroka gerezani mwaka 2006 nchini Yemen, na baadaye akachukuwa uongozi wa kundi la Al-Qaeda lililoko nchini humo.
CHANZO TRT SWAHILI
Chapisha Maoni