Mkali wa sinema za Kibongo Aunt Ezekiel akiwa na wafanyakazi wa Globalpublishers walipomtembelea kumuona mtoto wake.
Makubwa!
Aunt Ezekiel ameweka wazi kinachotafsirika kuwa ni kuzaa nje ya ndoa
huku akishikilia alichokiita ‘hayo ni mambo yake binafsi’, Ijumaa Wikienda liligaragazana naye kwa maswali.
Akizungumza
kwa njia ya simu na ‘kijumbe’ wetu wikiendi iliyopita, mkali huyo wa
sinema za Kibongo, alisema kamwe hapendi kuulizwa masuala ya ndoa yake.
Aunt Ezekiel na mume wake Moses Iyobo wakifurahia na mtoto wao.
Aunt
alisema suala hilo ni la kifamilia na kwamba yeye ndiye mwenye siri ya
nani baba wa mtoto huku akishindwa kukubali kama ni Sunday Demonte
ambaye ni mumewe wa ndoa, ndiye baba wa mwanaye Cookie.
“Mume
wangu anapaswa anisikilize mimi, hakuna mahali niliwahi kusema kuwa
mtoto huyu ni wa Iyobo (anayetajwa kuwa ni mpenzi wake), ni kweli
nimepiga picha na Iyobo tukiwa na mtoto, lakini mtu yeyote anaweza kuja
nyumbani, hata wewe (mwandishi), tukapiga picha nikiwa na mwanangu.
“Kuhusu
Demonte, huyo ni mtu wangu, siwezi kusema mtoto ni wa kwake na siwezi
kusema si wa kwake, ni mambo yangu binafsi, kama yeye (Demonte) akiamua
kufuata maneno ya watu, sawa lakini ni bora anisikilize mimi mkewe,”
alisema.
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida, Aunt alimlalamikia mwandishi wetu kwa
maswali mengi na mazito yaliyosababisha kukaukiwa maziwa kwenye matiti
yake na kwamba kwa wakati ule hakujua mwanaye Cookie angenyonya nini.
“Ona sasa, umeniuliza maswali mengi hadi maziwa yamenikauka, sijui mwanangu atanyonya nini?” alilalamika Aunt.
Chapisha Maoni