Uchaguzi wa ubunge
unaendelea nchini Burundi licha ya wiki ya maandamano ya ghasia dhidi ya
uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza wa kutaka kuwania muhula wa tatu.
Upinzani umesusia uchaguzi huo.Muungano wa Ulaya unasema kuwa uchaguzi huo utazidisha mgogoro uliopo.
Umoja wa Afrika umekataa kutoa waangalizi ukisema kuwa baadhi ya masharti yaliowekwa hayajaafikiwa kwa uchaguzi kuwa huru na haki.
Zaidi ya watu 70 wameuawa tangu mgogoro huo uanze.Karibu watu 130,000 wamelitoroka taifa hilo.BBC SWAHILI
Chapisha Maoni