0
Hillary Clinton aanza kujipigia debe Marekani
Kampeni za uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka 2016 zaanza nchini Marekani
Mgombea wa chama cha kidemokrasia Hillary Clinton amefanya mkutano wa kwanza wakampeni katika mji wa New York.
Mkutano huo ulioandaliwa na Hillary Clinton aliyewahi kuhudumu kama waziri wa mambo ya nje na ambaye ni mke wa rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton, ulivutia watu wananchi na vyombo vya habari.
Katika maelezo aliyotoa, Hillary Clinton aliwasilisha ujumbe wa kuleta ufumbuzi hasa katika matatizo ya kawaida.
Hillary Clinton aliomba kuungwa mkono kama mgombea urais kwa kutoa ahadi ya kuongezwa kwa mishahara ya wafanyakazi, kupunguzwa kwa kodi, utetezi wa haki za wanawake pamoja na ulinzi wa mazingira kwa ujumla.
Hata hivyo, Hillary Clinton hakugusia sana masuala ya sera na siasa za nje wala ulinzi na usalama wa kitaifa katika mkutano huo.
Miongoni mwa viongozi wanaowania nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya chama cha kidemokrasia wanaotarajiwa kuleta upinzani mkubwa kwa Hillary Clinton ni mkuu wa zamani wa mji wa Maryland Martin O'Malley na seneta wa Vermont Bernie Sanders

Chapisha Maoni

 
Top