0

Wito wa Angelina Jolie kwa nchi za Afrika
Muigizaji maarufu wa filamu nchinii Marekani, Angelina Jolie ametoa wito kwa nchi za Afrika kupinga unyanyasaji dhidi ya wanawake
Jolie ambaye pia ni balozi wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR, alishiriki katika mkutano wa Umoja wa Afrika uliofanyika siku ya Ijumaa huko Johannesburg, Afrika kusini.
Mkutano huo wa Umoja wa Afrika ulilenga kujadili suala la unyanyasaji dhidi ya wanawake duniani. 
Nyota huyo wa filam ya “salt” alisema kuwa tatizo hilo sio tu linalikumba bara la Afrika pekee bali ni dunia nzima kwa ujumla.
Aidha ameeleza kuwa kumekua na mikutano mingi ya kujadili jambo hilo lakini maendeleo ni madogo.
Jolie Alisema “Fikiria kama nchi zote 54 za Afrika zitaungana na kutoa sauti moja ya kupigania haki za wanawake, ni kwa kiasi gani zitakua zimesaidia jambo hili. Tatizo hili linaisumbua dunia nzima”.CHANZO:TRT SWAHILI

Chapisha Maoni

 
Top