
Mtu mmoja alifanya shabmbulio la kutumia silaha katika jengo la usalama huko Dallas, Marekani.
Muhusika wa shambulio hilo amejulikana kwa jina la James Boulware mwenye umri wa miaka 33. Hata hivyo vyanzo vya usalama vimeeleza kuwa haijabainika ni kundi gani la kigaidi ambalo James anahusiana nalo.
Polisi waliliona gari hilo na kumuona James akijaribu kuruka kwenye gari hilo lililokua na bomu.
Baadaye bomu hilo lililipuka kwenye gari ingawa polisi hawakukuta mabaki yake.
Polisi walimshambulia James na kumuua kabla hajatupa bomu lake. Hakuna mtu mwingine aliyeripotiwa kufa au kujeruhiwa. CHANZO:TRT SWAHILI
Chapisha Maoni