
Mvulana aliepandikizwa uume Afrika Kusini sasa ni baba mtarajiwa
Madaktari walioshuhulikia upandikizaji wa uume wa mvulana mmoja Afrika Kusini ambae alikatwa uume kwa bahati mbaya alipokuwa akikatwa jando, waliifahamisha familia ya kijana huyo kwamba mwenziwe wa kike ni mjamzito.
Daktari Van der Merwe alieongoza upandikizaji huo alifurahishwa na kufaulu kwa kazi yake na kusema kuwa asilimia 100 kwa 100 za hisia katika uume wa mvulana huyo zimerejea.
Mvulana huyo alikatwa uume miaka mitatu iliopita. CHANZO:TRT SWAHILI
Chapisha Maoni