Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk.
Willibroad Slaa akiwa na Mshauri wa Masuala ya Uchumi, Sayansi na
Maendeleo ya Jamii katika ulimwengu wa dijiti (digital), Dk. Mario
Voigt, walipokutana Villa La Collina, Milan kwa ajili ya kujadiliana na
kubadilishana uzoefu kuhusu namna bora ya kusimamia uchumi unaonufaisha
wananchi hususan kwenye nchi zenye utajiri wa rasilimali lakini watu
wake wanakabiliwa na umaskini, kama Tanzania. Dk. Voigt ni mtaalam
katika eneo hilo, akitokea iliyokuwa Ujerumani Mashariki, ambayo uchumi
wake ulikuwa ukiendeshwa na sera za kisoshalisti kabla ya kupitia
mabadiliko makubwa kutoka hali duni na sasa sehemu hiyo ni mojawapo ya
jamii zenye maendeleo makubwa ndani ya Ujerumani. Dk. Slaa yuko ziara ya
kikazi barani Ulaya kwa siku 7
Chapisha Maoni