
Hatimaye mgogoro wa ardhi wa zaidi hekta 200 baina ya wananchi wa chasimba na uongozi wa kiwanda cha saruji cha Twiga umemalizwa na waziri wa nyumba na maendeleo ya makazi Mhe.Wiliam Lukuvi akitangaza kubadili matumizi ya ardhi hiyo kuwa ya makazi yao kutoka mikononi kiwanda kama eneo la kuchimba madini.
Waziri Lukuvi ambaye ameandika historia katika mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya miaka 15 alifuatana na uongozi wa kiwanda,manispaa Kinondoni,Tanesco,mbunge wa kawe idara ya maji,piolisi na timu yake ya wizara akigiza eneo hilo kupangwa kama makazi ya wanachasimba ikiwemo miundombibnu ya maji barabara, shule,zahanati na huduma nyinginezo za kijamii.
Aidha Mhe.Lukuvui aliyeahidi kumaliza migogoro sugu nane katika jiji la Dar es Salaam pamoja kueleza kuutambua mgogoro huo tangu akiwa mkuu wa mkoa alikiri kushindwa kuingilia kati kutokana na sabambu mbalimbali na hatimaye kufikia nafasi ya dhamana ya wizara hiyo na kuamua kutimiza adhima ya serikali ya kuhudumia wananchi huku mbunge wakawe Mhe.Halima Mdee akikiri hatua iliyochukuliwa kuwa muafaka kwa serikali yoyote inayojali watu wake.
Kwa upande wake mkurugenzi wa kiwanda cha saruji cha Twiga Bw. Alfonso Rodrigoz pamoja na kukiri mgogoro huo kuwanyima usingizi kwa kipindi kirefu amempongweza waziri lukuvi na kuwataka wananchi kuanza ujirani mwema kwa maendeleo akiahidi kusaidia katika ujenzi wa miundombinu.
CHANZO: ITV TANZANIA
Chapisha Maoni