
Polisi
mkoani Iringa wamefanya msako kali kwa kushirikiana na vyombo vingine
vya ulinzi na uaslama na kufanyikwa kukamata magunia matatu ya bangi, CD
za mafunzo ya jihadi za kialshaababu pamoja na nguzo 35 za umeme mali
ya shirika la umeme Tanesco.
Alisema magunia hayo ya bangi yakiwa yamefungashwa katika mifuko mdogo na misokoto yalikamatwa pamoja na watuhumiwa sugu wawili.
“Watu
hawa wamekamatwa wakati wa kiendelea kufunga bangi hizo katika
vifungashio mbalimbali pamoja na misokoto,” alielezea kamanda.
Kamanda
huyo aliwataja watuhumiwa kuwa ni Steven Sanga na Nicolaus Tweve, ambao
alisema ni maarufu sana kwa kuingiza na kusambaza bangi mkoani hapa.
Alisema
kuwa Tweve ni maarufu sana kwa kuingiza na kusambaza madawa ya kulevya
mkoani hapa na hivi juzi juzi ametoka magereza kwa kosa hilo hilo la
kujihusisha na usambaji na uigizaji wa bangi.
“Watu kama hawa wanatuharibia vijana wetu, wanatuharibia pia nguvu kazi,” alisisitiza kamanda.
Kama
vile haitoshi, Jeshi la Polisi lilifanyikiwa kukamata nguzo za umeme
35, nyaya za umeme na vifaa vingine vya kufungia umeme katika maeneo
mbalimbali vinazodaiwa kuwa mali ya shirika la umeme nchini Tanesco.
Alisema
kuwa vifaa hivyo vimekatwa kwa watu binafsi wawili, lakini kutokana na
upelelezi kuendelea kamanda huyo hakutaka kuwataji watuhumiwa hao.
Aliongeza
kuwa nguzo hizo zilitakiwa kuwepo maeneo ya vijijini ambapo kuna zoezi
la kusambaza umeme vijijini, lakini zimekutwa kwa watu binfasi kinyume
na sheria.
“Huku ni kurudisha nyuma jitihada za serikali za kusambaza umeme katika mkoa wetu hasa maeneo ya vijijini,” alisema kamanda.
Wakati
huouhuo, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mbalimbali limewakata
watoto wanne wakiwa na CD zinazoonesha mafunzo ya ukatili, kuchinja na
kuua ya kialshaababu.
Alisema kuwa watoto hao wanakadriwa kuwa na umri kuanzia 12 hadi 16 na wanaonesha CD hizo katika maeneo mbalimbali.
Alisema
CD hizo zimekatwa kutoka kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu
na polisi inaendelea na uchunguzi kujua watoto hao wamezipata wapi na ni
kwa lengo gani na kutakujua baada ya mafunzo hayo watayafania kazi
gani.
“CD
hizo tumeziangali zinaonesha mafunzo ya kialshaababu yakiwemo kuua,
kuchinja pamoja na mambo mengine. CD hizi tumebaini zinaonesha kwa
kutumia kompyuta ambayo imefungwa kwa pasiwedi (password). Kama jeshi la
polisi hatutaishia hapo tutaendelea na uchunguzi watoto hao CD hizo
wanazipata wapi na kwa madhumini gani,” alisema.
Alisema
kuwa kumekuwepo na tabia ya watu kujihusisha na mambo ya kiuharifu kama
vile kusamabza madawa ya kulevya pamoja na uharibifu wa miundo mbinu ya
umeme.
Hata
hivyo, kamanda huyo ametoa wito kwa umma kushirikiana na jeshi la
polisi pamoja na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kutoa taarifa
pindi wanapoona kuna watu au vitu ambavyo si vya kawaida.
“CD hizi nyingi, bangi ni nyingi lakini vile vile uharibifu wa miuondombinu wa umeme ni mkubwa,” alimalizia kamanda.
Chapisha Maoni