
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza kwa msisitizo
juu ya jamii ya watanzania kuchukua hatua ya kuwalinda watu wenye
Ualbinism nchini wakati wa tukio maalum la maadhimisho ya siku ya
Kimataifa ya Uelimishaji Umma kuhusu Ualbino, iliyoandaliwa na tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini. kushoto kwake ni Wakili wa
Serikali na Mratibu wa masuala ya Albinism nchini, Bi Beatrice Mpangala.
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza kwa msisitizo
juu ya jamii ya watanzania kuchukua hatua ya kuwalinda watu wenye
Ualbinism nchini wakati wa tukio maalum la maadhimisho ya siku ya
Kimataifa ya Uelimishaji Umma kuhusu Ualbino. kulia ni maafis wa taasisi
hiyo ya UNESCO na kushoto kwake ni Wakili wa Serikali na Mratibu wa
masuala ya Albinism nchini, Bi Beatrice Mpangala.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bi Marry
Massay akisisitiza umma kuchukua hatua dhidi ya mapambano kwa watu
wenye Ualbinism kwa kuwalinda pamoja na kutoa elimu sahihi ya mapambano
ikiwemo kuachana na imani potofu dhidi ya jamii hiyo.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini
(DPP) Bi. Neema Ringo,akitoa wito kwa wadau mbalimbali (Hawapo pichani)
Kujitokeza katika kesi kutoa ushahidi hasa wakati wa kesi dhidi ya
vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa watu wenye Albino nchini.ambapo
alieleza kuwa wamekuwa na changamoto dhidi ya mashahidi hivyo ni wakati
sasa wa wananchi kujitokeza kufuatilia kesi hizo ikiwemo mashahidi
kujitokeza.
Mmoja wa wadau waliojitokeza kwenye maadhimisho yaliyoandaliwa na
tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini, akichangia maoni yake
dhidi ya hatua za kufanyika ili elimu ifike kwa jamii ikiwemo kuwatumia
watu mbalimbali hasa ngazi za chini wakiwemo Wenyeviti, madiwani na
wakuu wa Wilaya na Mikoa.
Mmoja wa mdau wa masuala ya haki za binadamu, ambaye ni mlemavu,
akichangia mada kwenye kwenye maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini, yaliyofanyika jijini Dar es
Salaam.
Taswira katika mkutano huo wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ukiendelea ukumbini hapo...!
Na Andrew Chale, modewjiblog
Tume ya Haki za binadamu na Utawala bora
nchini, leo Juni 13,2015, imeungana na watanzania wote kuadhimisha siku
ya Kimataifa ya uelimishaji umma kuhusu Ualbino na haki za watu wenye
Ualbino ambapo imeitaka jamii kutambua haki na wajibu wa kuwalinda na
kuwathamini.
Akisoma taarifa maalum kwa wadau mblimbali
na waandishi wa habari waliojitokeza jijini Dar Es Salaam, Kamishna wa
tume hiyo, Dkt. Kevin Lothal Mandopi alieleza kuwa jamii inayo wajibu wa
kuwathamini watu hao wenye albinism kwani nao ni kama binadamu wengine
na wana haki sawa.
Kamishna Mandopi katika taarifa hiyo
alibainisha kuwa, mpango wa elimu kwa umma umelenga kubadilisha fikra,
mtazamo na imani potofu juu ya watu wenye ualibinism.
“Ni dhahiri kuwa iwapo jamii itaelewa dhana
nzima ya Ualbinism na kubadili fikra na dhana potofu dhidi ya watu hawa,
kuna uwezekani mkubwa wa kukomesha kabisa matendo maouvu dhidi ya ndugu
zetu wenye Ualbinism” alieleza Kimishna Mandopi.
Kwa upande wake Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
Bi. Zulmira Rodrigues alisisitiza jamii nchini kuongeza upendo pamoja na
kuachana na imani potofu inayosababisha kukithiri kwa vitendo hivyo
hapa nchini.
Pia alibainisha kuwa, imefika wakati sasa wa
kutoa elimu ya kutosha kwa jamii ilikutambua wenye Ualbinism ilinao
waishi na kupata haki sawa kama binadamu wengine.
“Wajibu wetu ni kuwathamini na kuwalinda
watu wenye Ualbinism, tumetembea maeneo mbalimbbali ikiwemo Kanda ya
Ziwa katika vituo maalum vya watoto wenye Albinism, Ni wakati wa
kuendelea kutoa elimu ili watoto hao watoke huko ili waishi na jamii
kama wengine” alisisitiza Bi. Zulmira.
Kwa upande wake, Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala
Bora, Bi Marry Massay alizitaka mamlaka husika ikiwemo za Serikali na
watu binafs, vyombo vya habari na jamii kwa pamoja kutoa elimu ya
uelimishaji umma kuhusiana Ualbinism ilikuendelea kuwa Tanzania yenye
amani na upendo kama ilivyojizolea sifa ndani na nje ya mipaka yake.
Naye Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya
Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) Bi. Neema Ringo, alibainisha kuwa,
ofisi yake imekuwa mstari wa mbele kufuatilia kesi mbalimbali ikiwemo
dhidi ya jamii ya wenye Albinism huku akiwataka wananchi kujitokeza
kutoa ushahidi pamoja na kufuatilia kesi hizo mara kwa mara.
Kwa upande wa wadau wengine walitaka
Serikali kuwa mstari wa mbele kushikamana na jamii hiyo yenye ualbinism
ilikutokomeza kabisa imani potofu iliyojijengeka kwa watu ikiwemo kutoa
elimu kwa ngazi zote mara kwa mara.
Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ndiye mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya
kimataifa ya kuongeza ufahamu juu ya Ualbino ambayo yameandaliwa na
Chama Cha Albino Tanzania, jijini Arusha.
Chapisha Maoni