0
Raia mweusi auawa na Polisi Marekani
Polisi wamuuwa raia mmarekani mwenye asili ya Afrika mbele ya watoto.
Taarifa hizo kuhusu kifo cha raia huyo zilifahamisha kuwa Polisi walimfyatulia risasi mbele ya watoto zaidi ya 50.
Afisa mmoja wa Polisi aliyefahamika kwa jina la Antonia Torres ambae alikwa akifanya kazi katika ukumbi wa Gibson kwa muda wa miaka 20, alimfyatulia risasi mtu mmoja mwenye umri wa miaka 40 akidhani kuwa nondo aliyokuwanayo mkononi ni silaha.
Tukio hilo lilitokea kipindi ambapo watoto walikuwa wakicheza katika kambi ya michezo ya kipindi cha kiangazi.

Raia huyo aliyeuawa alifariki papohapo katika eneo la tukio.

Kamanda wa Polisi, Rodolfo Llanes alifahamisha kuwa uchunguzi utafanyika ili kubainisha sababu zilizopelekea polisi huyo kufyatua risase.CHANZO TRT SWAHILI

Chapisha Maoni

 
Top