0
Rais wa Madagascar aapa kutimiza ahadi alizotoa kwa wananchi
Mahakama kuu ya katiba yafutilia mbali ombi la kumtaka rais wa Madagascar kujiuzulu
Rais wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina, ametoa wito wa ushirikiano kwa wananchi ili kusaidiana na serikali katika shughuli za kuleta maendeleo nchini.
Rais Rajaonarimampianina alitoa maelezo hayo baada ya mahakama kuu ya katiba kufutilia mbali ombi la kumtaka kujiuzulu lililowasilishwa na bunge.
Akielezea kupata funzo kubwa kutokana na hatua hiyo iliyochukuliwa na wabunge,Rajaonarimampianina alisema, ‘‘Suala hili limenisaidia niweze kujirekebisha hasa katika masuala ya uongozi. Nitawajibika kikamilifu ili nitimize ahadi za wananchi wa Madagascar.’’
Rajaonarimampianina amekuwa akishutumiwa na kutakiwa kujiuzulu kutokana na kushindwa kutimiza ahadi alizotoa kwa wananchi tangu kipindi cha uchaguzi mkuu wa 2013.
Wabunge 121 kati ya 151 waliwahi kupiga kura kumtaka Rajaonarimampianina kujiuzulu mnamo tarehe 26 mwezi Mei. CHANZO TRT SWAHILI

Chapisha Maoni

 
Top