0
Vituo 150 vya tiba dhidi ya ulevi Iran
Iran yatangaza kufunguwa vituo 150 vya kutoa matibabu dhidi ya ulevi wa kupindukia
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na shirika la afya la Iran ni kwamba zaidi ya watu 150,000 ni walevi wa kupindukia. 
Iran imechukuwa uamuzi wa kufunguwa vituo hivyo ili kupambana dhidi ya madhara ya ulevi ambayo hivi sasa yamekuwa tatizo kubwa katika jamii.

Wahusika katika shirika la afya la Iran lililifahamisha shirika la habari la Isna kuwa tatizo la ulevi wa kupindukia limekuwa tatizo katika jamii ambalo limekuja na kuibuka kwa kasi.

Alireza Norouzi ambaye ni daktari katika kituo cha kutoa matibabu kwa watumiaji wa vilevi alifahamisha kuwa, katika kituo chake kutatolewa mafunzo kwa watu watakaopewa tiba dhidi ya ulevi.

Kituo cha kwanza cha matibabu dhidi ya ulevi kilifunguliwa kwa mara kwanza jijini Tehran mwaka 2013.

Chapisha Maoni

 
Top