WATU 43 WAUAWA NA BOKO HARAM NIGERIA
Wanamgambo wa Boko Haram walivamia vijiji vitatu katika jimbo la Kano na kuwauwa watu 43.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na mashahidi wa tukio, walifahamisha kuwa wanamgambo hao walitumia pikipiki kuvamia vijiji hivyo nakuendesha shambulio hilo.
Boko Haram ilipora mali za wanakijiji.
Shirika la habari la AFP lilifahamisha kuwa baadhi wa manakijiji walifaulu kukimbia katika vijiji jirani.
CHANZO TRT SWAHILI
Chapisha Maoni