0
Zaidi ya watu 100 wauawa  Iraq

Zaidi ya watu 100 wauawa kutokana na shambulizi la anga Iraq

Zaidi ya watu mia wakiwemo wanawake na watoto wameuawa na wengine wengi wamejeruhiwa katika shambulizi la angani katika mji wa Hawiji kijiji cha Kirkuk kusini mwa Iraq.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mwanahabari wa Al Jazeera Nasser Shadid, alisema kuwa mashambulizi hayo yalilenga soko kuu na daraja lililoko mjini.

Kwa taarifa kutoka kwa wananchi wa kijiji hicho, kuwa wanaamini kuwa shambulio hilo limefanywa na ndege za kijeshi zilizotengenezwa na Urusi aina ya “Sukhoi.
CHANZO TRT SWAHILI

Chapisha Maoni

 
Top