RAIS WA SUDANI ATAFUTIWA KIBALI CHA KUKAMATWA NA POLISI WA AFRIKA YA KUSINI
Mkurugenzi wa shirika lenye makao makuu yake mjini Johannesburg Kaajal Ramjathan-Keogh, alinukuliwa na vyombo vya habari nchini akisema kuwa alikuwa amepokea taarifa ya kutafutwa na Mahakama ya kimataifa rais wa Sudani al-Bashir.
Rais al-Bashir, amekuwa rais wa kwanza katika orodha ya marais wanaotafutwa na mahakama ya kimataifa baada ya kesi kusikilizwa na kutolewa kibali cha kukamatwa.
Al-Bashir, anashukiwa kwa makosa matano ya uhalifu dhidi ya ubinadamu (mauaji, kuteketeza kizazi, uhamishaji kwa kutumia nguvu, mateso ya ubakaji).
Na pia anashukiwa makosa mengine mawili ya uhalifu wa kivita (mashambulio ya moja kwa moja dhidi ya raia) katika jimbo la Darfur nchini Sudan.CHANZO TRT SWAHILI
Chapisha Maoni